Dini nchini Kenya kwa jumla zinaishi kwa amani, ingawa miaka ya hivi karibuni baadhi ya Wakristo waliuawa na wafuasi wa Al Shabaab.
Upande wa takwimu, kulingana na sensa ya mwaka 2009, asilimia 82.5 ya wakazi wa Kenya walikuwa Wakristo (asilimia 47.4 Waprotestanti, asilimia 23.3 Wakatoliki, asilimia 11.8 Wakristo wa madhehebu mengine mbalimbali), asilimia 11.1 ni Waislamu, asilimia 1.6 ni wafuasi wa dini za jadi, asilimia 1.7 ni wa makundi mengine ya dini, na asilimia 2.4 wanadai hawana uhusiano na dini yoyote ile.[1]